Monday, November 17, 2014

magauni na mashati ya makenze

kwa wale ambao wamekuwa wakiangaika kutafuta mishono kwa ajili ya vitenge aina ya makenze sasa limepata ufumbuzi kwani Dfashion imewaletea mishono mizuri ya magauni na mashart ya vitenge hivyo,  kazi ni kwenu sasa kutathimini upi umeupenda 







Tuesday, September 2, 2014

mazoezi kwa ajili ya kupata hipsi

Kuliko kutumia kemikali katika kujipata shepu nzuri ni bora ukafanya mazoezi ambayo baadae ya kutakupatia shepu nzuri unayoiitaji 
 kuna mazoezi mbalimbali  yanayokuza na kuyapa makalio na nyonga muonekano mzuri, zoezi mojawapo ni

’’squarts’’ yaani kuchuchumaa kwa kiswahili rahisi. Kufanya squarts, waweza tumia uzito au waweza fanya squarts bila kutumia uzito wowote. Unachukua uzito unaoweza kuhimili, na kuuweka mabegani (kumbuka uzito huu unatakiwa uwe umewekwa pande zote kwa uwiano sawa ukiunganishwa na bomba ambalo ndiyo unaliweka mabegani). Simama wima miguu yako ikiwa imetengana kiasi, halafu chuchumaa taratibu, na kunyanyuka taratibu. Rudia mzunguko huu mara 6 mpaka 8, kwa kila seti, na ni vema kufanya seti tatu mpaka tano. Kumbuka waweza fanya squarts bila kuwa na uzito wowote, cha muhimu ni kuikutanisha mikono yako pamoja nyuma ya kichwa wakati wote unapokuwa unachuchumaa na kusimama. Ni muhimu kufahamu kwamba, kama unataka sehemu zako za makalio kuongezeka ukubwa, basi ni vema kutumia uzito.




kwa leo naomba niishie na zoezi moja, zoezi jingine msikose kutembelea blog hii kesho ambapo mtaweza kujione mazoezi mengine mbalimbali 

Thursday, August 21, 2014

Friday, August 15, 2014

maids dress

kwa msichana yeyote ambaye anatafuta mshono kwa ajili ya mates, Dfashiontz imewaletea mishono mbalimbali kwa ajili ya mates 




Tuesday, August 12, 2014

mibano ya nywele

kwa mdada yeyote mwenye nywele ndefu ama ameshonea nywele bandia (weaving ) na umekosa mbano wa nywele zako, Dfashion inawapa mibano mbalimbali kwa ajili ya nywele zenu. kazi ni kwenu kuchagua mbano 
utakaoupenda 
  





Monday, August 11, 2014

Mavazi ya asili barani Africa

katika bara la Africa kuna nchi nyingi, na ndani ya nchi hizo kuna tamaduni zinazotofautisha nchi  hizo ili  kuzifanya  kuwa za kipekee. Katika swala zima la mavazi, kila nchi ina vazi lao la asili ambapo huwafanya kuonekana wa kipekee wawapo nje ya nchi yao.
vazi la nchini Ghana 


vazi la nchini Nigeria 


vazi la South Africa



 vazi la Zambia

hatuna budi kuziehimu, kuzitunza, na kuziendeleza  tamaduni za nchi, kwani kwa kufanya hivyo hufanya nchi husika  kuonekana ndani na nje ya nchi