Sunday, August 3, 2014

njia asili ya urembo

Haya warembo kuna njia nyingine ya asili ya kuufanya uso wako kuwa laini na wenye kuvutia, njia hiyo si nyingine bali ni matumiz ya papai 

jinsi ya kutumia 

Chukua papai likate kisha toa mbegu alafu  lisage kwa kutumia blenda
au pondaponda kwenye kibakuli kwa kutumia  mchi mdogo wa
kinu, kisha weka mchanganyiko huo kwenye chombo ulichokichagua .Vunja yai na koroga  kwa pamoja kuhakikisha kuwa mchanganyiko huo umechanganyika vizuri. Safisha uso wako kwa kutumia cleanser au maji ya vuguvugu na uondoe uchafu wote ulioganda usoni. Kisha paka mask kuzunguka uso wako, na unapopaka hakikisha kuwa, mchanganyiko huo haugusi macho yako. Osha uso wako baada ya dakika 15 kwa kutumia maji ya vuguvugu. Jifute kwa kutumia taulo safi .

Chanzo urembo

0 comments:

Post a Comment