Tuesday, September 2, 2014

mazoezi kwa ajili ya kupata hipsi

Kuliko kutumia kemikali katika kujipata shepu nzuri ni bora ukafanya mazoezi ambayo baadae ya kutakupatia shepu nzuri unayoiitaji 
 kuna mazoezi mbalimbali  yanayokuza na kuyapa makalio na nyonga muonekano mzuri, zoezi mojawapo ni

’’squarts’’ yaani kuchuchumaa kwa kiswahili rahisi. Kufanya squarts, waweza tumia uzito au waweza fanya squarts bila kutumia uzito wowote. Unachukua uzito unaoweza kuhimili, na kuuweka mabegani (kumbuka uzito huu unatakiwa uwe umewekwa pande zote kwa uwiano sawa ukiunganishwa na bomba ambalo ndiyo unaliweka mabegani). Simama wima miguu yako ikiwa imetengana kiasi, halafu chuchumaa taratibu, na kunyanyuka taratibu. Rudia mzunguko huu mara 6 mpaka 8, kwa kila seti, na ni vema kufanya seti tatu mpaka tano. Kumbuka waweza fanya squarts bila kuwa na uzito wowote, cha muhimu ni kuikutanisha mikono yako pamoja nyuma ya kichwa wakati wote unapokuwa unachuchumaa na kusimama. Ni muhimu kufahamu kwamba, kama unataka sehemu zako za makalio kuongezeka ukubwa, basi ni vema kutumia uzito.




kwa leo naomba niishie na zoezi moja, zoezi jingine msikose kutembelea blog hii kesho ambapo mtaweza kujione mazoezi mengine mbalimbali